Wimbo mtamu nim’shindwa,
Ingawa maneno yan’winda…
Zan’kimbiza pote niendapo,
Hata kichwa nik’twaa kwenye mto.
Wimbo mtamu nim’shindwa,
Mwindaji huyu kawindwa…
Silali, sili, sij’tambui,
Hadi lini hata mie sijui!
Wimbo mtamu nim’shindwa,
Kichwa kitambo kishetulizwa…
Kuandika siandiki na wino…
Ni hisia hunitoza nyimbo.
Wimbo mtamu nim’shindwa,
Kama binti aliyeapizwa…
Mgongo nimechoka kuupinda…
Baraka niongezee eeh Maulana!
Advertisement



Jitahidi usishindwe,
Nikidhani,
wimbo mtamu hufariji!
Asante kwa kunipa moyo Dada…missed youB-)