Masika yamepita,
Mawazo hayajaisha,
Hata macho nikiyafumba…
Bado nakutazama,
Hata kichwa vipi nikilikuna…
Bado nakuwaza,
U mawazoni n.m.
Masika yamepita,
Mawazo hayajaisha,
Hata macho nikiyafumba…
Bado nakutazama,
Hata kichwa vipi nikilikuna…
Bado nakuwaza,
U mawazoni n.m.
Dada Serina umesema,
mawazo yapo daima,
tena daima na daima,
mpaka kichwa chauma,
na kufikiri u´kichaaa
mawazo.
u mawazoni usiku na mchana…..
umeutawala moyo kwa sana….
u mawazoni nirudie tena….
sababu mi nakupenda sana….
ni wewe mwinginewe sijamwona…
Sasa serina jamni MASIKU ndio nini?
Asanteni nyote kwa maoni yenu… Luihamu, habari ya masiku?
Jua lachomoza, mpaka linazama,
bado nazidi kukuwaza,
maumivu nayasikia,
katika moyo yanavyokata,
sugu chapitiliza kidonda,
kamwe sijutii kupenda,
ipo siku nitakupata,
kila ninachotaka,
hakika nitakipata.
Umuwazaye sana
…Eni Emu
Kwa heshima na taadhima
…Eni Emu?
Pasi shaka ushaelewa hitaji langu
…Eni Emu?