Umeniweza…

5 05 2009

Naamka na tabasamu,

Maana najua wewe ni wangu,

Hisia zinazonipitia kwangu,

Furaha tupu, mwenzangu!

Napendelea unavyonipapasa…

Kwa maneno zilizo na ladha,

Natikirinywa na lako tabasamu…

Ujuzi ushaigundua wa kunipa hamu,

Na kumbatio lako mwenzangu…

Humtuliza shetani wa kiume wangu!

Huyu shetani wangu wa kiume…

Amejua nani ndie mme,

Keshawafukuza wengi nakwambia …

Kila umbo kutoka kila daraja,

Maskini, tajiri, vijana , wazee,

Warefu, wafupi, weusi na weupe,

Lakini sasa naamka na tabasamu…

Na sio maneno tu hunifanya,

Nikalala na tabasamu…

Umeniweza!


Actions

Information

12 responses

5 05 2009
Ria

Hi!

Good to see you’re back :D

This seems to explain a lot as to your disappearing act LOL as you say, kweli amekuweza haha and I wish you a life full of tabasamus :D

5 05 2009
Ria

Just had to read this again.
Kumbe una shetani wa kiume? That’s an excuse I may start using soon as well! I thought it was just your temperment ;)

6 05 2009
Mwanasosholojia

Ama kweli amekuweza!
Shetani wako amekumaliza!

6 05 2009
ringojr

serina,
kuwezwa na amekuweza ni maneno mawili tofauti.
kuweza ni kwakipindi kilichopita na amekuweza ni kwakipindi kilichopo
who knows about kesho kama atakuweza? au wewe ndio utamuweza au yeyote watawezana.

Changamoto tu Serina.

amani.

6 05 2009
Simon Kitururu

DUH!

6 05 2009
Serina

@ Ria: Thanks! I actually believed it was a severe case of PMS :)

@ Mwanasosholojia: Shetani wangu amenisaidia kuchuja!

@ Ras Lui: Naishi kwa ya leo… na kwa leo, ananiweza :D

@ Simon: DUH! maanake nini?

6 05 2009
ringojr

duh!!! makubwa.

6 05 2009
Fadhy Mtanga

Umeniweza vile navotaka,

Hakika leo sina tena mashaka,

Niwapo nawe siishi kuburudika,

Napata nguvu hata nihisipo kuchoka,

Umeniweza hadi mtima kusisimka,

Kila uchao nazidi kuhamanika,

Umeniweza!

Ni nyongeza tu da Serina.

6 05 2009
Serina

@ Fadhy: Asante kwa nyongeza!

8 05 2009
Simon Kitururu

@Serina : Duh! maana yake ni DUH!:-)

8 05 2009
bomseh

You are tagged. Visit mine for details and comply.

11 05 2009
Serina

Bomseh…noted.

Leave a comment