Tembea, tembea usichoke…
Tembea uone dunia,
Uyaone ya ulimwengu
Tembea ufuate riziki,
Tembea ukawaone marafiki,
Tembe, tembea…
utafute pesa,
utafute mali,
utafute amani,
utafute penzi,
utafute unachotaka kutafuta.
uridishe moyo wako…
hujafungwa pingu,
hujakalishwa kitako…
Tembea, tembea…
Tembea uende shughulini,
mapato lazima siku hizi,
Nenda sokoni, dukani,
zilizobaki pitishia
‘grocery’ na kisha nyumbani
Tembea, tembea…
Kiguu na njia…
Tembea na nia.


ama kwa hakika “Mwenda bure si sawa na mkaa bure”, tembea uone!
MAKUBWA!!!DUH
Lakini Serina kuna wale wanaolala na kuletewa.
serina siku hizi uko busy sana,kwani tenzi zimepungua sana si kawaida yako au?
Duh !!
@ Subi, Karibu.
@Luihamu, wajua maisha bwana….
Nice. My motto: Tembea.
Tembea wala usichoke,
Kokote kule ufike,
Riziki yako uidake,
Nyumbani waridhike,
Tembea, tembea.
@Kaasa, Wise girl
.
@ Fadhy, Karibu.
Serina malenga wetu
Unagusa mioyo yetu
Kuzisoma akili zetu
Kuzirusha beti kwetu
Nami nipo matembezini
Natembea hapa duniani
Kwa sasa nipo masomoni
Nchi ya watu ughaibuni
Hii yote ni kutembea
Vitabu kuvisomea
Nyumbani bongo kurejea
Taifa letu kujengea
Nakukaribisha buloguni
Wala sikuweki kapuni
Sitakutupa asilani
Wewe kwangu ni fanani!
Tembea tembea,
kijiweni nimejikuta,
kwa Serina nachangia.
siku zilipita,
mashairi hatukuyapata.
sasa nayafurahia,
kimoyomoyo najiimbia.
Kwa nini kuhadithiwa,
tembea utajionea.
@ Mwanasosholojia na Kissima, karibuni na asante.
Bora umerudi Serina…
Rudi bloguni…
“Kiguu na njia…
Tembea na nia.”
Thanks for the advice!
@ Bwaya: Asante
@ Ria: Don’t take it personally.