Tembea, tembea…

29 04 2009

Tembea, tembea usichoke…

Tembea uone dunia,

Uyaone ya ulimwengu

Tembea ufuate riziki,

Tembea ukawaone marafiki,

Tembe, tembea…

utafute pesa,

utafute mali,

utafute amani,

utafute penzi,

utafute unachotaka kutafuta.

uridishe moyo wako…

hujafungwa pingu,

hujakalishwa kitako…

Tembea, tembea…

Tembea uende shughulini,

mapato lazima siku hizi,

Nenda sokoni, dukani,

zilizobaki pitishia

‘grocery’ na kisha nyumbani

Tembea, tembea…

Kiguu na njia…

Tembea na nia.