Ni nani aliyejua,tabiri nyota utakwenda peponi/ahera?
angali mchanga,ukafundwa
ukatosheka,ukaishi.
Walikudharau ewe nyota
wakasahau uchangia mwanga palipo na kiza
walikuona mlalahoi.wima
kama mtaa wa mchamba wima.
Hukusikiliza ya wapitao
hukujali ya wapitao
hukunun’gunika kama wapitao
ewe nyota ulikunjwa na kufundwa.
Ukajisahau kutoa mfano mzuri kwa wadogozo
wapitao tena wanakuita zozo
licha ya kuwa nyota.
Wadudu hao umewavaa
wadudu hao wamekuvaa
na sasa wagagaa
chali wajiburazaa.
Dakika za lala salama
ukakumbuka shuka
wenzio kumekucha
wewe wakumbuka shuka,wakati
kichwa kilishazama.
Sikusemi nyota,bali nakukumbuka nyota
kila kiza kiingiapo ‘n’ takukumbuka nyota
nakupenda nyota
wasalimu huku uliko,wafundishe yale tulopende utufunze
nami nifundwe.
Luihamu 2009


Vipo kama nyota vyang’aa,
Binadamu kavingaza,
Angani vyaangaza,
Kama vyota vyatokeza.
Wajuaje hiyo ulodhani nyota,
Kumbe i zile dutu za kisayansi?
Nyota alale salama,
hakutaka enda kwa usalama,
sasa kimemkuta kiama…
Jua lajiwakia,
kipi cha kusingizia,
nyota yako ulijiamulia,
wa jua mwanga ukaukandia,
ona ahera pakungojea,
huna tena cha kujutia,
na gramu moja wajiondokea,
safari ya milele nakutakia,
mwanga jua halikukubania,
uzembewo utaujutia,
maisha ulipaparikia,
kila la heri unakoelekea.
Usiuume mkono unaokulisha!
Jag har varit här förut, jag älskar dikter. Kommer också mer att hälsa på
Du är varmt välkommen hit Yasinta! Vi behöver fler kvinnliga röster/jämnställhet
Jag är ganska upptagen nu och skriver inte så mycket som jag skulle vilja!
En gång till, varmt välkomen!
Ama, kumbe humu na kiingereza cha Sweden / Denmark nacho kimo? Ntaanza kumwaga ki-Spanish kwenye blog za watu. Lol
Jamani nawapenda na ninafurahia uwepo wenu
DUH!
@ Mubelwa: Gracias
@ Simon: ???