Nimetosheka

10 03 2009

Shughuli hapa na pale zaniita…

Kuzitimiza bila malalamiko desturi,

Ulegevu huu umetoka wapi?

Maungo kwa machofu nimevunjika,

kama mganga anayepunga pepo kilingeni…

Mwisho wa simba umeletwa na nzi!

.

Hapa nasema, pale nakimya…

Jogoo la shamba haliwiki mjini…

Ongeza kasi, jua latua…

Huu ni uvivu wa kike au ni balaa?

Maliza ya leo, leo… ya kesho mageni

Hivi kumbuka walipwa masaa

Lakini tena…

Sheria hazitii wasiwasi aliyetosheka!

Nimetosheka.


Actions

Information

6 responses

11 03 2009
bwaya

Kutokuridhika ndiyo ya mwanadamu asili
Ukishiba sasa njaa itakupa akili
Ili kesho na ule kufanza mzunguko kamili

Utoshekapo fikiri

Hujatosheka utagundua

Kwani kutokutosheka ndiyo asili

11 03 2009
ringojr

umetosheka?
hajatosheka…
najikwamua kwa leo
najituma kwa/ya leo
nitajitahidi kwa leo
pochi,mshiko,midikodiko
jah ahsante.

amani.

11 03 2009
Marvin K. Tumbo

“Mwisho wa simba umeletwa na nzi”

That is a mighty good line…

Nimejaribu kuandika kama wenzio hapa juu lakini Kiswahili imegonga ukuta.

How’s that?

Great Poem…

Regards

11 03 2009
Ria

Umenikumbusha wahindi wanaoajiri wafanyikazi nyumbani kwao kisha kuwaambia wachambue vitunguu saumu karibu gunia nzima kila wiki baada ya kazi ya nyumbani.Vituko vyao nilipata kujua kutoka msichana anayenisaidia kazi nyumbani kwangu sasa. Eti kila saa ilikuwa, harakisha, harakisha, sitakulipa kuketi nde!

12 03 2009
Serina

@ Bwaya: kweli: lakini kugundua saa zingine hutokea kiajali :)
@ Ras Lui: Maisha hayo… kuna, ukunwe.
@ Marvin: Nendelea hivyo hivyo… hatua moja ikifuatwa na nyingine.
@Ria: Ukoloni mambo leo (Neocolonism)!

12 03 2009
Global Voices Online » Kenya: The Big Language Dilemma For Kenyan Poet Bloggers

[...] a poem called ‘Nimetosheka‘ (I am fed up) she says, Shughuli hapa na pale zaniita… Kuzitimiza bila malalamiko desturi, [...]

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Connecting to %s




Follow

Get every new post delivered to your Inbox.