Kitoto kichanga…
Hukaribishwa na wengi,
‘kishezaliwa tu! safari huanza!
kuishi duniani mkondo wa kwanza.
Wengine safari, kwao huwa fupi…
waliobakia nao mola awanusuru!
kulingana na sheria za wengine ataishi
Hawezi chagua…
mlezi wake duniani,
Hawezi chagua…
kati ya ukafiri na dini.
Amri zifuatwe bila ubishi!
Sio wote hubahatika…Safari hii kuimaliza.
Wengine safari huwa fupi…
wengine ndefu…
wengine safari ya furaha…
wengine safari ya matatizo.
Kisha baleghe…
Uamuzi mikononi mwake…
atakavyoishi ye…
na wengine wanaouhusiano naye,
atakavyofanya ye…
atakavyojitetea jangwani.
Wengine wana safari ngumu…
iliyojaa majaribio na mahangaiko,
Wengine safari, starehe tupu!
Waishije maisha yako?
Wanungunika?
Watesa?
Wateseka?
Wayafurahia?
Kufa…
wengine hujipangia…
wengine hupangiwa…
Kaka husema,
Kuzaliwa bahati…
Kufa lazima.
Nd’o maisha hayo!


Maoni