Kukimya kwangu…
sio kumaanisha sina la kusema
maoni sitaki tu kutema
macho zaidi yan’tazama
Kukimya kwangu…
sio kumaanisha maneno sina
hotuba si neno geni ni tabia
moyoni hata hivyo najiimbia
Kukimya kwangu…
sio kuwa wa kusema nae sina
usifikirie kuwa ni ujinga
na tena ujue sio kuringa
Kukimya kwangu…
sio kumaanisha sijui nitamke vipi
bado sijafungwa ulimi
macho nayo bado usingizi
Kukimya kwangu…
ni njia ya kujifunza tena nakwambia
masikio niliyojaliwa yanapata kusikia
walio na lakunena nafasi nawapatia
Kukimya kwangu…
najua ni unyonge wangu
na pia ni nguvu kwangu
hilo lako jibu mwenzangu
Kukimya kwangu…
ni kusema kwangu.

