Vitu nane msizojua kun’husu

23 07 2007

In’bidi niandike tena

Kwa kuwa um’nena

Vitu nane wataka kujua

Vitu nane nit’watambulia

Nimalizapo mi’ kusema

Zamu nanyi m’tapewa

Vitabu ni la kwanza,

hunionyesha mwangaza

Pili, napenda upekee

lakini sio upweke

Kujivunia upishi wangu namba tatu

kuridhisha wengine raha yangu

Nne, marafiki nawathamini

Bado sijajua ni kwa nini

Tano, useremala nim’jaribu

mbao nim’pasua bila aibu

Hata hivyo mazingira nayajali

namba sita sio kwa ajali

Nafasi ya saba naipa ndoto

maisha mazuri kwa wote watoto

La nane mjaze wenyewe

au tuseme tu ni uzembe

Watu nane … zamu yenu

Mwandani

Da Mija

Kitururu

Issa Michuzi

Ras Luihamu

Mentalacrobatics

Mwenye Macho

Ndesanjo (sio zile za Ethan…zingine)

na nane mkishewachagua

msisahau pia kuwajulisha


Actions

Information

7 responses

24 07 2007
Simon Kitururu

Serina , haka kashughuli kweli !:-)

25 07 2007
kipusa

this is the first blog i’ve read in swa. will be back for more

25 07 2007
Serina

@ Simon: shughuli si kitu kizuri?
@ kipusa: karibu.

25 07 2007
luihamu

Serina you caught me unawareness,it was like shaggy with his song IT WASNT ME,

Nilibaki nikicheka tu,na kushangaa

hongera,Serina unakumbuka mchezo wa SHAKE,NADHANI SHAKE NA TAGGED ni brain challenge.

25 07 2007
Serina

:-) Nami nilipatikana kwenye hali hiyo hiyo

27 07 2007
Mentalacrobatics

Hehe finally managed to get my list up! Thanks for the tag!

10 08 2007
MAVITU NANE KUHUSU MIE « MWENYE MACHO

[...] kuandikiwa na Serina nikiambiwa niainishe vitu nane kuhusu [...]

Leave a comment