Heri niishi bila wewe

29 07 2007

Tafadhali zungumuza taratibu

Hata! sitosongea karibu

La sivyo watatusikia

Na kugundua kwanini sikuamini

Mapigo yakishekuwa desturi

Paza sauti mwenzangu

maanake sikio halisikii

Msamaha wamuomba nani

Asiyelala genezani

Kutokana na wako shetani

Wasiwasi unanizunguka

Ni wapi nitapindukia

Unachotaka sikupatii

Kuna mengi hatujayatatua

Kabla mme sijakutii

Mda wetu ulipotelea wapi

Kipenzi ulinipenya vipi

‘Kaniwacha na utupu moyoni

N’naogopa ushavunjika

Maanake sikuweza vumilia

Matumaini yashadidimia

Huwezi nishawishi

Na wala sitaki kujua

Presha sitaki ipande

Heri niishi bila wewe





Vitu nane msizojua kun’husu

23 07 2007

In’bidi niandike tena

Kwa kuwa um’nena

Vitu nane wataka kujua

Vitu nane nit’watambulia

Nimalizapo mi’ kusema

Zamu nanyi m’tapewa

Vitabu ni la kwanza,

hunionyesha mwangaza

Pili, napenda upekee

lakini sio upweke

Kujivunia upishi wangu namba tatu

kuridhisha wengine raha yangu

Nne, marafiki nawathamini

Bado sijajua ni kwa nini

Tano, useremala nim’jaribu

mbao nim’pasua bila aibu

Hata hivyo mazingira nayajali

namba sita sio kwa ajali

Nafasi ya saba naipa ndoto

maisha mazuri kwa wote watoto

La nane mjaze wenyewe

au tuseme tu ni uzembe

Watu nane … zamu yenu

Mwandani

Da Mija

Kitururu

Issa Michuzi

Ras Luihamu

Mentalacrobatics

Mwenye Macho

Ndesanjo (sio zile za Ethan…zingine)

na nane mkishewachagua

msisahau pia kuwajulisha





Pepo bado i kavu

12 07 2007

Jibu la Pepo Kato Sio Kavu, na Marazzmatazz

 

Vizuri umeketi ukadhamiri

Ya daftari pamoja na ya akilini

Kuwa ya dunia siyathamini

Na hamna yeyote ninayemwamini

Asilimia tisainitisa wala zaidi

Kweli usemavyo uchujaji naujua

Hisia zim’kuwa vigumu kuz’fafanua

Ulimwengu kanifunza roho yangu sitofungua

Hamna kama wewe anayenifahamu

Chanzo cha utesi wangu

Mashauri yenye faida bado natafuta

Gumzo na furaha bado zaniepuka

Hisia kuzibania sijui pakupinduka

Upweke, machozi wala hazijamwagika

Duh! Naona bado sijazinduka

Mawimbi baharini kun’ mazuri na mabaya

Kuvuma na kutulia kama waimbaji kwaya

Hupanda na hushuka bila kuelekezwa

Mengi zaidi ya hisia na ndoto sitazitaja

Daima ukavu usije’mi kunipata

Wasema ukavu huu si ukavu

Bali mfano tu kama vile ndoto

Nd’o maanake pepo kavu nikauita

Maana bado n’natumaini kuwa utapita

Mzibaji mwanya at’kapojitokeza

Hisia sizikatai wala sizikani

Majina kuyabandika wala si kazi

Nasubiri at’kaye kaa nami ufukoni

Mtandoni, maktabani na pia mkahawani

Najua siku itafika…lakini sijui lini

Ucheshi wako, utesi wangu

Duh! Kweli kama zamani