Mbona maisha kama pepo kavu?
Usin’ambie kila pepo na m’da wake,
ulimwengu ushanifunza….
Nini n’nalokosa lakini n’nachotamani?
Starehe ya kuketi na kupiga gumzo la kimaana…
Starehe ya kupiga gumzo na mtu aliyekomaa…
Chemchem la mawaidha yenye busara,
Mawazo tasa tukawa tumeyawacha nyuma…
Lakini ucheshi tusiutupilie mbali,
Mshindo wa bahari na mawimbi….
Kwenye miguu yetu tun’poketi ufukoni…
Hali ya anga likibadilika,
Maktabani au mkahawani sawa pia….
Sio kila siku mtandoni….
Niambie sasa,
Ukavu huu utaisha lini?
mchezo wa kuwindana sina mda nao…
tamaa uli’oamsha atautekeleza nani?
Yu wepi at’kaye zima kiu yangu?
Mwanya huu atauziba nani?
Maoni