Namlilia malkia

7 02 2007

Namlilia jirani,

Alikuwa malkia.

Kamkosea nani,

asiye na hisia?

Usiku wa juzi,

Kanieleza yote…

Jinsi aliv’ofikia uamuzi,

Kuwa kalemewa na vyote.

Chini ya mnazi…

Kapatikana Kesho yake.

Kazibwa mdomo,

hatukumsikia…

Kafungwa mikono,

hak’weza ‘jitetea…

Kachapwa viboko,

kawachwa kalegea…

Namlilia jirani,

malkia miongoni mwa malkia.