Kam’ kawaida,
kuwaza na kuwazua…..
nini kipya wauliza?
sina mapya…
matumaini tu!
N’natumaini kuwa u nuru yangu,
Utanionyesha njia wakati wa giza
Utanionyesha mbele n’napofika mwisho
Utaniliwaza n’naposhikwa na msiba
N’natumaini kuwa hutan’peleka mrama,
hata kam’ tum’gombana,
hata kam’ tum’koseana,
hata kam’ tun’ maswala ya kindani
yanayosababisha mapambano.
N’natumaini kuwa hut’nipa kamba,
un’ambie n’ende zangu.
Nim’pokea kamba nyingi maishani mwangu,
n’lizorundika kwenye sitoo,
nafikiria kushona mkeka
n’tauweka kwenye shoo.
N’natumaini matumaini yangu,
Hayat’kupa unyonge…

