Jenga nyumba yako
unavyotaka,
tumia udongo au matofali
makuti, mawe au glasi
jenga nyumba uwezano nayo
kifedha
kimuda
kisifa
jenga nyumba itakayo onyesha
ubinafsi wako
‘kisha jenga nyumba,
panda mti kando yake
mti ambao utafaidhika nao…
kwa matunda au kivuli,
au pahali ambapo
nyani na ndege
wanaweza tua na kupata riziki
kwa kukunyelea kichwani,
unapopumzika wewe
kivulini.
tend’keza nyumba yako
na utend’keze mti wako
lakini usisahau ukaupanda
mpakani mwa nyumba
kwa nini wauliza?
mizizi hatari
zitanyemelea polepole
na kubomoa nyumba’ko
sifa zote ul’zopata
zitapotelea kwenye kicheko
cha maadui, marafiki
majirani na hata wapita njia
“kafikiria nini yule?
hakujua mizizi hatari?”


Maoni