Mwenzangu,
hujanisahau
umen’pa moyo
Kila n’napokuwaza
unan’pa moyo
kazi un’yofanya
usiku na mchana
umen’pa moyo
jinsi unav’ong’ang’ana
kukuri kakara
umen’pa moyo
mlango wa kwanza
wa pili na tama
umen’pa moyo
kwa majaribio na raha
machache na mahaba
umen’pa moyo
kwa kun’chekesha na kun’tania
kunielekeza bila kuniangusha
umen’pa moyo
hili langu dua,
akubariki Mola,
na Akupe moyo.

