Mwenzangu

30 10 2006

Bilauri kwenye sinia
hugongana
lakini
hazivunjiki
Penzi langu kwako
hivyo hivyo,
mwaka nenda,
mwaka rudi.
Miaka kenda na bado nahesabu

Najaribu kukusahau
tabasamu lako
mavazi yako
mwendo wako
Najaribu,
usiku na mchana
kuachana
kupatikana
na huzuni uliodua tulipoachana

Maji mengi yamepita
chini ya daraja
mengi,
masafi
machafu
mazito
cha muhimu
daraja bado lipo
na twasimama hapo hapo.

Penzi kikohozi
halifichiki
wajijua
mbona washuku