Buriani Mzazi Mwenza

16 12 2009

Mganga wangu, mzazi mwenza…

Umetuacha na machozi,

Umetuacha na majonzi…

Umemuacha binti akiuliza,

Maana ya maisha ni nini?

Hata kama tulishetengana,

Binti katufunga kama kamba…

Buriani Shahame,

Buriani mzazi mwenza…





Mo Faya indeed!

4 12 2009

Sikudhania nitapata kushuhudia mambo kama yale niliyoyaona jana kule Go Down… sizungumuzii kuhusu onyesho lenyewe la Mo Faya lakini kuhusu wapangaji.

Tuliwasili pale baada ya kazi, mwendo wa saa moja hivi… tukawakuta watu wengi wamekusanyika pale nje… Kisa na maana… ubalozi wa Netherlands umelipia viti vyote kwa hivyo, wapangaji walionelea ya kuwa sie tusio wageni wa ubalozi, turudishiwe hela zetu au tukubali tikiti za siku nyingine… nakwambia… Mo Faya ikaanzia hapo!

Kama wewe ni mkaazi wa Nairobi, wafahamu hali ya barabara ilivyokuwa jana… msongomano wa magari kila ulengapo jicho… kwa mfano, nilitembea kutoka kazini hadi mjini katikati…nikatafuta teksi ya kunifikisha Go Downs… kawaida huwa dakika kumi hivi lakini jana ilichukua saa nzima hivi… kisha niambiwe eti sitapata kutazama Ma Faya?????

DUH!

Tulipiga kelele sana… waandalizi hawa husema ya kuwa wakenya hawajitokezi kuwapa motisha wenziwao sana sana katika haya maswala ya usanii….Mbona walituuzia tikiti basi kama ubalozi ulikuwa umeshalipia viti vyote? Tikiti si agano kati yangu na wao… tulikwamilia hapo hapo na kuwaambia waite polisi basi maana kilichotuleta hapo, kwa ahadi kati yetu (Tikiti) ni Mo Faya na sio kula chakula kilichandaliwa kule ndani, wala kutazama wazungu waliokuwa wamejaa kule… tukakataa katakata kukubali kurudishiwa hela za gharama zetu…

Tulifaulu. Tukaingia. Tukatazama Mo Faya. Tukafurahia. Tukaondoka.

UKOLONI MAMBOLEO POTELEA MBALI!!!!





Mo Faya

3 12 2009

After getting a taste of Kenyan talent the other day at Open Mic, which was a lot of fun (thanks Mr. Adolwa) we are psyked up for Mo Faya, the Musical by Eric Wainaina tonight…  (Just google it to read the reviews… will probably be too wired up afterwards to write one)





End of year slam… Poetry competition!

30 11 2009

Am I looking forward to the end of year slam tomorrow at Club Soundd…. hopefully there will be a few familiar faces there and good poetry!!! and laughter of course!!!





Kiswahili Wikipedia Challenge

19 11 2009

Jishindie…

bonyeza hapa kwa maelezo